Gigy Money Atangaza Rasmi Hana Rafiki, Ni Baada ya Wote Kushindwa Kutokea Alipojifungua - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Atangaza Rasmi Hana Rafiki, Ni Baada ya Wote Kushindwa Kutokea Alipojifungua

Mwanadada Gigy Money ametangaza kuwa kwa sasa hana rafiki kwa sababu aliyokuwa akiwategemea kama marafiki zake wameshindwa kujitokeaza hata kumpa nepi katika uzazi wake na kusema kuwa wamesahau kuwa alikuwa akiwasaidia kwa zaidi ya miaka saba mjini lakini leo hii kama vile hawajui kilichotokea kwake.

Katika ukurasa wake wa instagram, Gigy Money ameonekana kukerwa na baaadhi ya rafiki zake wa kike waliojifanya kuwa marafiki lakini sasa hivi wanakuwa hawajui kuwa amejifungua , aliandika

“Thanks aunty missa i love you shoga,jamani wengine mnajifanya mashost , twin boo , bae ila nepi tu zinawashinda natangaza rasmi sina shoga mjini hapa ni washkaji tu byee, #ushoagakazinaujuekujitoa.

Kwa hesabu za haraka haraka marafiki wa karibu wa Gigy money ni pamoja na Amber Lulu pamoja na Tunda ambao walikuwa karibu nae , ingawa madongo haya hayajaweka wazi yamemlenga nani lakini ni marafiki wa karibu wa Gigy money.


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.