Fainali ya Ligi ya Mabingwa Kuoneshwa Bure, Fahamu Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Kuoneshwa Bure, Fahamu Hapa

Ikiwa tayari zimesalia siku chache tu ambapo macho na masikio ya kila mpenda soka duniani yataelekezwa mjini Kyiv, Liverpool watakuwa wakicheza dhidi ya Real Madrid katika mchezo huu kumpata bingwa wa Champions League msimu huu kutoka Uwanja wa NSK Olimpiyskyi mjini Kyiv, Ukraine.

Iko hivi, Shirika la michezo la BT Sports limeamua kuuonesha mchezo huu bure kabisa, kupitia channel yao ya Youtube, BT Sports wataonesha mechi hii moja kwa moja kutoka mjini Kiev na ni data tu ndizo utatumia.

Katika fainali ya msimu uliopita ya Champions League kati ya Real Madrid vs Juventus BT Sports walivutia jumla ya watazamaji 6.5m dunia nzima na wanaamini safari hii uwepo wa klabu toka Uingereza utaongeza watazamaji.

Katika kutanua wigo wa kuongeza watazamaji, mchezo huu pia utaoneshwa katika application ya BT Sports pamoja na website yao, na yeyote mwenye app hiyo ataweza kuuona mchezo huo moja kwa moja kutoka mjini Kyiv, Ukraine.

Peter Oliver ambaye ni mkurugenzi wa BT Sports amekiri kwamba uwepo wa Liverpool katika fainali hii ni fursa kubwa katika biashara ya uoneshaji mpira na wataitumia fursa hiyo kuongeza mashabiki dunia nzima.

Tarehe 26 mwezi huu ndio siku ambayo wababe hawa wawili watatoana jasho, timu zote mbili zimeshindwa kuchukua ubingwa katika ligi zao za ndani na hii inaweza kuwa nafasi yao kuweka heshima.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.