Ebitoke: Sijaumia Bikira Yangu Kuondolewa, Dunia ya Kujivunia Bikira Imepita - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ebitoke: Sijaumia Bikira Yangu Kuondolewa, Dunia ya Kujivunia Bikira Imepita

Mchekeshaji kutoka Timamu, Ebitoke amedai bikira yake kuondolewa na muimbaji Ben Pol sio ishu kwenye maisha yake kwani kipindi cha mwanamke kujivunia bikira kimeshapita.

Akiongea akiwa Kikaangoni ya EATV, Ebitoke amedai kilichotokea katika maisha yake juu ya mahusiano na Ben Pol sio kitu kibaya, kwani wakati yupo naye mapenzi yalikuwa moto moto hivyo aliitendea haki nafsi yake.

“Kweli bikira yangu imetoka lakini sijaumia hata kidogo, maisha ya sasa yamebadilika, sasa hivi sio kama zamani bila bikira hauolewi,” alisema Ebitoke “Yote niliyopitia nikiwa na Ben Pol ni sehemu ya maisha yangu, sijawahi kujuta kwa sababu najua nimpata mwanaume mwingine,”

Katika hatua nyingine amewataka mashabiki wa vichekesho vyake kukaa mkao wa kula kwaajili ya filamu yake mpya itakayotoka mwakani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.