Dogo Janja, Uwoya Wakesha Kusaka Mtoto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja, Uwoya Wakesha Kusaka Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya wanatafuta mtoto.

Uwoya ambaye tayari ana mtoto mmoja Krish aliyezaa na marehemu Ndikumana Kataut amedai yuko katika jitihada za kumtafutia Krish mdogo wake.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, kwa nyakati tofauti mastaa hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala hilo kwa nguvu zao zote.

"Tupo bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,” alisema Dogo Janja

Lakini pia Uwoya naye alifunguka na kusema ni haki yake kumpatia mtoto mume wake kama wanandoa lakini hasa hivi sasa anahitaji kumpa mdogo wake Krish kwani ameshakuwa mkubwa.

" Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake“.

Irene Uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwaka jana mwishoni. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.