Dogo Janja Akubali Kumuita Mtoto wa Uwoya Mdogo Wake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja Akubali Kumuita Mtoto wa Uwoya Mdogo Wake

Msanii wa muziki bongo Dogo Janja ambae mwaka jana alifunga ndoa na mwanadada Irene Uwoya na watu wamekuwa wakimsema sana tangu wao kuwa katika mahusiano kutokakna na ukweli kwamba wawili hawa hawalingani kiumri na kwamba watu wamekuwa wakimlinganisha Dogo Janja na Irene kama mtu na mtoto wake.

Katika siku ya kuzaliwa ya mtoto wa uoya wa kiume anaejulikana kwa jina la Krish, Dogo Janja aliamua kuwaridhisha walimwengu baada ya kumuita Krish kuwa ni mdogo wake na kwamba irene uwoya ni mama yao na kumshauri mdogo wake huyo kuwa msikivu kwa mama yao na kwamba anamshauri kutulia na kumheshimu mama yao.

Katika ukurasa wake wa instagram, Dogo Janja aliandika "happy birthday mdogo wangu Krish , Mungu akupe maisha marefu sana mama anatupenda watoto wake wote tusimuangushe."

Posti hiyo ilizua maswali na maneno engi katika kursa za instagram lakini wawili hao wamekwa wakionekana kuwa na mapenzi yaliyoshibaban kuliko hata vile ambavyo watu wengi walikuwa wakisema kuwa ndoa hiyo haitachukua muda mrefu kwa sababu wawili hao wamependana kwa kimaslahi na sio mapenzi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.