Diamond na Vanessa Mdee Kuwania Tuzo Uingereza - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond na Vanessa Mdee Kuwania Tuzo Uingereza

Wasanii wanaofanya vizuri katika kutangaza muziki wa Bongo ndani na nje ya nchi ambao kwa sasa wamekuwa kama kaka na dada wa bongo fleva Vannesa Mdee na Diamond Platnumz wameingia katika headlines tena baada ya kuwekwa tena katika tuzo za huko uingereza wakiwa na wasanii wengine wakubwa Africa.

Tuzo hizo za African Pride 2018 zitakazofanyika June 3 mwaka huu kutakuwa na wasanii wengine wengi kutoka Afrika ambao watachuana vikali na wasanii wetu kutoka Tanzania.

Wasanii kama Tiwa Savage, Yemi Alade, Kiss Daniel , Patoranking, Davido, Wizkid na wengine wengi watakuwepo kutafuta msanii bora wa muziki Afrika kwa upande wa kike na upande wa kiume.

Vanessa na Diamond sio mara yao ya kwanza kuwania tuzo mbalimbali za nje ya nchi na kutoka na ushindi wa kuipa Tanzania heshima kwenye muziki, hivyo kila la kheri kwa wasanii hawa lakini pia pale wanapohitaji sapoti kutoka kwa mashabiki tuwape ili wafanye vyema na kuleta ushindi nyumbani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.