Billnass Amgeukia Alikiba, Fahamu Zaidi Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Billnass Amgeukia Alikiba, Fahamu Zaidi Hapa

Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambaye anampa ushirikiano mkubwa kwa kila jambo ambalo huwa analifanya katika harakati zake na kudai siku zikikaribia huenda wakatoa wimbo wa pamoja.

Billnass ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 jioni baada ya kuonekana picha katika mitandao za kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa studio katika siku za nyuma kidogo.

"Nina mahusiano mazuri na Alikiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu hata muda mwingine huwa tunataniana, naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma huwa ananiambia mdogo wangu hapo fresh au kazia buti sehemu fulani. Inshallah panapo majaliwa nitafanyakazi na Alikiba ila kwa sasa sitaki kuliweka wazi suala hili, ila watu wajue tu kuwa tunamawasiliano mazuri baina yetu",
amesema Billnass.

NAFASI YA KUSHINDA MAPESA KILA SIKU, >>BOFYA HAPA<< KUJISAJILI

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.