Baada Ya Video Ya Alikiba Kubaniwa Youtube Amefunguka Haya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada Ya Video Ya Alikiba Kubaniwa Youtube Amefunguka Haya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Alikiba amefunguka kuhusiana na ngoma yake mpya ya Mvumo wa radhi aliyoiachia siku ya Ijumaa.

Kumekuwa na taarifa kuwa Alikiba amefanyiwa figisu figisu na watu fulani kwani tangu Jumamosi Kumekuwa na na tatizo la views (watazamaji) wamekuwa hawaongezeki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amerikiri tatizo hilo na kusema kuwa wanafanya jitihada kadhaa ili suala hilo likae sawa:

"Tunafahamu tatizo la kutokuongezeka kwa views kwenye akaunti ya YouTube ya ALIKIBA, na tupo kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya YouTube Africa ambao wanafanya kila jitihada kutatua tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo. Shukrani kwa uvumilivu wenu na support mnayoendelea kutupa! Endeleeni kuangalia video ya Mvumo wa Radi".

Video ya Mvumo wa Radi tangu jana Mei 12, 2018 imekuwa namba moja kwenye Trending ya video zinazotazamwa zaidi Tanzania na mpaka sasa bado ipo namba moja lakini tangu jana licha ya kuwa namba moja bado views wanaongezeka taratibu sana ukilinganisha na siku ya Ijumaa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.