Zari Amkomesha Diamond, Atua Bongo na Kuondoka Bila Kukanyaga Madale - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari Amkomesha Diamond, Atua Bongo na Kuondoka Bila Kukanyaga Madale

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss lady’, aliyekuwa baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’, amekinukisha ile mbaya baada ya kutua Bongo na kutokwenda nyumbani kwa jamaa huyo, Madale-Tegeta jijini Dar, risasi Jumamosi limenyetishiwa.

 ATUA USIKU WA MANANE, AFIKIA HOTELINI

Zari alitua Dar usiku wa manane wa Jumanne iliyopita na kufikia katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro, zamani Kempinski iliyopo Posta, Dar na mapema kesho yake (Jumatano iliyopita), alisaini dili nono na Kampuni ya Softcare. Zari alisaini dili hilo la mamilioni, tukio lililofanyika mbele ya vyombo vya habari kwenye ukumbi wa hoteli hiyohiyo na sasa akawa ndiye balozi mkuu wa pampers za watoto zinazosambazwa na kampuni hiyo.


AULIZWA KUHUSU DIAMOND

Katika zoezi hilo la kusaini dili hilo, ulipofika muda wa maswali, Zari aliulizwa juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo ‘aliwaka’ na kusema kwamba, kilichomleta Bongo ni dili hilo tu na asingependa kuzungumzia mambo ya Diamond.

AWA BENETI NA NOEL, ATIMKA BONGO

Tofauti na alivyozoeleka kuwa na Diamond, safari hii Zari alionekana akiwa beneti na jamaa ambaye ni mbunifu wa mavazi Bongo aliyetajwa kwa jina moja la Noel kabla ya kutimka Bongo mara tu baada ya kukamilisha kilichomleta.


TAARIFA ZILIVYOTUFIKIA

Tukirudi nyuma, usiku uleule wa Jumanne, mara tu baada kutua kwa mwanamama huyo, taarifa za uwepo wake Dar zilienea, nasi zikatufikia.

Tulipomtembelea kwenye kurasa zake za kijamii ndipo tukakutana na ujumbe wake kwenye Snapchat akithibitisha kuwepo Bongo kwa shughuli hiyo maalum. Usiku huohuo, pia baadhi ya watu walikosa usingizi huku wakivipa vidole vyao kazi ya kuandika na kuposti kwenye mitandao ya kijamii juu ya ujio wa Zari ambaye aliishia hotelini.

NI WIKI KADHAA TANGU AMMWAGE DIAMOND

Zari alilifanya jambo hilo ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipotangaza kummwaga rasmi Diamond ambaye kwa sasa makazi yake, mama na ndugu zake ni Madale-Tegeta jijini Dar.

FAMILIA YA DIAMOND

Taarifa za kijasusi kutoka ndani ya familia ya Diamond huko Madale-Tegeta, nje kidogo ya Jiji la Dar, zilidai kwamba, familia hiyo ilikumbwa na sintofahamu na kujikuta ikiparanganyika na kila mmoja kusema lake kutokana na kutokuamini kama kweli Zari anaweza kuwa Dar, lakini asikanyage nyumbani hapo kuwasalimu. “Achilia mbali kuwasalimu, lakini bado chumba chake hakina mrithi pale Madale na hata yeye mwenyewe alisema ameachana na Diamond, lakini undugu utaendelea kuwepo kwa sababu amezaa naye watoto wawili, Tiffah na Nillan.

MAMA DIAMOND ATIBUKA

“Kiukweli jambo hilo limetuumiza sana sisi kama familia, yaani kila mtu ana mtazamo wake, lakini Zari ametutibua sana,” alisema memba huyo wa familia ya Diamond na kuongeza: “Unaambiwa bi mkubwa (mama Diamond) ametibuka balaa maana anaona kama Zari hathamini wala hajali kama amezaa na mwanaye. “Bi mdanga (mama Diamond) anahoji kama Zari amegombana na Diamond ndiyo awachunie wote?”

MAWIFI WATOA YA MOYONI

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, dada zake Diamond au mawifi wa Zari, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ na Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’, walitoa ya moyoni; esMa PlaTNUMZ “Mimi ninachojua Zari hawezi kuja Madale kwa sababu amegombana na Diamond. Kwanza mimi sina ukaribu naye kwa sababu kama una wifi, alafu

akawa anakufanyia vitu vizuri, anakujali na kukunyenyekea, lazima uwe karibu naye, mi’ sina ukaribu naye,” alisema Esma Platnumz ambaye kwa muda mrefu alidaiwa kutoivana na Zari kwa kuwa anampenda zaidi Wema Sepetu aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla ya Zari.

QEEN DARLEEN 


“Mi’ sina cha kusema, lakini watu wajue tu ninampenda sana Zari, tena sana,” alisema Queen Darleen ambaye tangu zamani alijipambanua kuwa anamkubali Zari. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.