Zari Afunguka 'Siwezi Kudate Mtanzania Tena', Adai Mwanaye Sio wa Tandale - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari Afunguka 'Siwezi Kudate Mtanzania Tena', Adai Mwanaye Sio wa Tandale

Mfanyabiashara maarufu na baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kuapa kuwa hataweza kutembea na mwanaume wa Kitanzania tena.

Zari ameyasema hayo baada ya Kupitia kipindi Kigumu na Ex wake Diamond ambaye alichepuka sana kipindi cha Mahusiano yao ya miaka minne hadi kufikia hatua ya kuzaa nje.

Zari alimmwaga Diamond mapema mwaka huu siku ya wapendanao baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Lakini pia Zari ameibuka na kudai kuwa mtoto wake Tiffah sio wa Tandale hii iliyokea siku chache zilizopita wakati Zari na marafiki zake walipokuwa kwenye Instagram live.

Zari alifunguka na kusema mtoto wake Tiffah anashindwa kutofautisha kati ya R na L tabia ambayo ameirithi kutoka kwa Upande wa Baba yake kwani Watanzania wengi hawawezi kutofautisha R na L na wengi wao wanamuita Zali badala ya Zari.

Ndipo mmoja kati ya marafiki wa Zari alisema Tiffah ni wa Tandale Lakini mara moja Zari alikataa na kusema mwanaye sio wa Tandale.

Tandale ndipo Diamond na familia yake walipokulia na hajawahi hata mara moja kukataa asili yake na hata albamu yake inaitwa ‘A boy From Tandale’.


PAKUA APP YETU MPYA ILIYOBORESHWA USIPITWE NA HABARI ZETU FASTA KILA SIKU >>BOFYA HAPA<<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.