Wema Sepetu: Tuzo Zangu Zimewatoa Povu, Sasa Nina Hasira Ya Kufanya Kazi Nzuri - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu: Tuzo Zangu Zimewatoa Povu, Sasa Nina Hasira Ya Kufanya Kazi Nzuri

Msanii wa Bongo movie Wema sepetu amefunguka tena kuhusiana na wasanii wenzake kumtolea povu baada ya kujishindia tuzo mbili kama msanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Wasanii kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna wasanii  wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.

Baada ya povu hilo Wema amewajia juu wasanii hao na kuwataka waache wivu kwani yeye amestahili tuzo hiyo kwa movie yake ya heaven sent kwani imeleta changamoto kwa wasanii wenzake.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Wema alifunguka haya:

"Kwanza kikazi kidogo tu cha heaven sent kimeleta maneno haya...kwahiyo wamenitia hasira na pia wamenifanya nione kuwa mimi ni tishio kwao, alafu huyo mtu ambaye anaongea nimesha fanya naye kazi alafu tumeshawahi kuwa karibu 

"Mimi sina tatizo na yeye nashangaa kwa Nini imekuwa hivi halafu nimeshafanya naye movie na nimemnyoosha kwenye kazi ambayo tumefanya lakini sijawahi kusema kitu chochote kibaya juu yake”.

Wema ameongeza kuwa kinachosababisha mpaka mambo yanakuwa hivi ni wasanii wa Bongo movie kuoneana wivu ambao unasababisha kunakuwa hakuna umoja kati yao hali inayosababisha tasnia hiyo kurudi nyuma.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.