Wema Sepetu Atoa Kauli Hii Kuhusu Kifo Chake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Atoa Kauli Hii Kuhusu Kifo Chake

Msanii wa filamu za Bongo Movie Wema Sepetu amerudi tena kwenye headlines huku safari hii akishangaza watu wengi baada kusema akifa anataka watu wapendeze kwenye msiba wake.

Msanii wa Bongo fleva Shilole alisema kuwa siku ya msiba wake anataka aagwe kwenye msikiti na sio Leaders Club ambako watu wanakaa na kunywa na kufanya starehe nyingine.

Wema naye ameibuka na kudai kuwa akifa anataka kwenye msiba wake watu wapendeze wavae vizuri na wafurahie maisha aliokuwa anaishi lakini pia anataka jeneza lake lipambwe kwa maua ya pinki.

"Napenda sana siku ya mazishi yangu waombolezaji wawe kwenye muonekanao mzuri na pia sehemu ambayo mwili wangu utafikia pawe pamepambwa vizuri kwa maua ya pinki yanayovutia,” alisema Wema.

Staa huyo alifunguka zaidi kuwa kwenye mazishi yake hayo baada ya familia, mtu mwingine ambaye anataka awe mstari wa mbele kwenye mazishi yake ni staa mwenziye, Aunt Ezekiel na kudai kuwa yeye ndio ataweka ua wa kwanza kwenye kaburi lake kabla ya staa mwingine yeyote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.