Vanessa Mdee Afunguka Haya Baada ya Video Yake ‘Wet’ Kufikisha Views Milioni 1. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee Afunguka Haya Baada ya Video Yake ‘Wet’ Kufikisha Views Milioni 1.

Japo imekuwa siyo jambo geni tena kuona video ya Bongo Flava kufikisha views milioni moja YouTube lakini imekuwa siyo kazi rahisi kuweza kuifikia namba hiyo hasa katika kipindi kifupi zaidi.

Basi Vanessa Mdee amefikia namba hiyo kupitia video ya wimbo wake mpya ‘Wet’ ambao amemshirikisha G Nako tena ndani ya wiki mbili pekee.

Msanii huyo hakutaka jambo hilo liweze kumpita kiurahisi bila kutoa neno lolote. Vee Money kupitia mtandao wa Instagram amewashukuru mashabiki wake huku akiongeza kuwa kufikisha views hao kwake ni kitu kikubwa sana.

“1Million views in 2 weeks #Wet Kwangu mimi ni kitu kikubwa tena sana, (nimesema KWANGU MIMI). Aiseeee nakushukuru wewe uliyoitazama hii Video ni FURAHA KUBWA kwangu na team nzima ya @mdeemusicofficial much love to you,” ameandika Vanessa Kwenye mtandao huo.
Hii ni video ya nne ya Vee kufikisha views milioni moja baada ya ‘Cash Madame’ (1.8m), ‘Kisela’ (2.1m) na ‘Juu’ aliyofanya na Jux (2.3m).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.