Umewahi Kujiuliza Kwanini Ndege Nyingi Zimepakwa Rangi Nyeupe ? Jibu Hili Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Umewahi Kujiuliza Kwanini Ndege Nyingi Zimepakwa Rangi Nyeupe ? Jibu Hili Hapa

Kama umewahi kupanda au kuiona ndege, utakuwa umegundua kuwa ndege nyingi zina rangi nyeupe. Hata kama zimepakwa rangi nyingine lakini rangi nyeupe haiwezi kukosa

Umewahi kujiuliza kwanini ndege nyingi zimepakwa na kuwekwa nakshi kwa rangi nyeupe ?

1- Sababu za kisayansi: rangi nyeupe husaidia kupunguza joto ndani ya ndege kwasababu rangi nyingine hufyonza mwanga na kuongeza joto ndani ya ndege, jambo ambalo linapaswa kuliepuka

2- Urahisi wa kukagua nyufa na hitilafu: Ndege hukaguliwa mara kwa mara hivyo ni rahisi kubaini nyufa na hitilafu kwenye tabaka la ndege kwasababu kasoro huonekana ndege ikipakwa rangi nyeupe.

Sio sababu zote ni za kisayansi kuhusu ndege kuwa na rangi nyeupe. Zipo sababu zingine ambazo haziwezi kupuuzwa. Mfano wa sababu hizo ni:

Kupaka rangi ni gharama: Katika taaluma ya usafiri wa anga, kuipaka rangi ndege sio sawa na kupaka rangi ukuta wa nyumba. Inahitaji uwekezaji wa fedha, rasilimali watu na muda.

Rangi nyeupe huongeza thamani ya ndege kwenye soko

Ikiwa umeipaka ndege yako rangi tofauti na nyeupe kwa madhumuni ya kuuza, tarajia kupata bei ya chini ukilinganisha na ndege yenye rangi nyeupe.

Rangi nyeupe haififii haraka: Ikiwa ndege itapaa angani, inapita kwenye hali ya hewa tofauti tofauti na kama haina rangi nyeupe, muonekano wake utafifia haraka ambapo wamiliki watalazimika kuipaka rangi mara kwa mara ili kung’alisha muonekano wake. Ndege nyeupe ikiwa angani haionyeshi utofauti hata kama itakaa angani kwa muda mrefu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.