Steve Nyerere: Akataza Watu Kwenda Kumwona Majuto Kwa Lengo Tu La Kupigana Nae Picha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Steve Nyerere: Akataza Watu Kwenda Kumwona Majuto Kwa Lengo Tu La Kupigana Nae Picha

Msanii wa filamu nchini Tanzania na mwanasiasa Steve Nyerere amefunguka na kuwataka wasanii wenzake na watu mbalimbali wasiende hospitali kumuona Mzee Majuto kwa lengo la kupigana nae picha ili atakapo kuwa amefariki waweze ku-post aliyopiga nae bali waende kumuona kwa ajili ya kuombea dua.

Steve ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuonekana wasanii na watu maarufu mbalimbali wakionekana kuweka picha mitandaoni pindi walipokuwa wamekwenda kumtembelea Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini Jijini Dar es Salaam ambapo amelazwa mwanzoni mwa wiki hii kutoka na maradhi yake ya tezi dume yanayomuandama.

"Twendeni tukamuone Mzee Majuto, tusiende kumuona Majuto kwa ajili ya kupigana nae picha kwa sababu wengi akili zao zinawaza kuwa atatutoka 'atafariki' mambo hayo ni ya Mwenyezi Mungu. Wengi wanahofu kwamba akishafariki aweze kuwa na picha aliyokwenda kumuona, naomba tufute hayo mawazo", amesema Steve Nyerere

Pamoja na hayo, Steve ameendelea kwa kusema "hakuna mtu yeyote duniani aliyesema kwamba kuumwa ni kifo bali kuumwa ni ibada tu, inakukumbusha kuna Mungu. Kwa maana hiyo tusiende hospitali kwa lengo la kupiga picha, twendeni hospitali kwa ajili ya maombi yatakayomfanya mwenzetu asimame na michango kuhakikisha Majuto anachangiwa".

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.