Siri ya Diamond Kuchaguliwa Kombe la Dunia Yavunja - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siri ya Diamond Kuchaguliwa Kombe la Dunia Yavunja

Mara nyingine labda watu wamekuwa wakijiuliza kwanini Diamond achaguliwe katika Kombe la Dunia kuiwakilisha Afrika na wala sio wasanii wengine waliopo Afrika, mbona kuna wasanii wengi tu wakubwa mbao wamekuwa wakifanya vizuri sana lakini hawajachaguliwa mpaka amechaguliwa Diamond.

Raia mmoja kutoka Afrika Kusini ambae ni mdau mkubwa wa muziki barani Afrika anafunguka na kusema kuwa yeye ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta wasanii watano kutoka Afrika watakao shiriki kutengeneza wimbo wa kombe la dunia na kutokana na vigezo alivyo kuwa navyo Diamond haikuwa rahisi kuacha kumchagua.

Tim Horwood anasema kuwa Diamond ni moja kati ya wasanii waliojenga ngome kubwa sana barani Afrika kupitia muziki wake kiasi kwamba hata alipopewa kazi hiyo hakuweza kuacha kumfikiria Diamond Platnumz.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.