Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 5) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 5)


Riwaya: MSAMAHA WA MAMA 
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 5

Niliongea kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nilishahisi kuna kitu nimemkosea mme wangu na mimi nlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.

Nilipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husda mpaka nliogopa, alionekana kuwa mtu aliejawa na hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia " SIITAJI KUZAA KWA SASA HIVI..

Ni jibu ambalo lilinifanya jasho lianze kunitoka kabla hata ya kumuuliza kwa nini, nlihisi tumbo linauma, mwili wote uliishiwa nguvu, nlitoa macho na kumuuliza kwa sauti ya upole.
"Kwa nini hutaki kuzaa?.
"Siitaji maswali, bali nimekwambia sitaki kuzaa nielewe mwanamke!. alinijibu hivyo baada ya kumuuliza.

Alitoka akaingia chumbani, nlijaribu kumuita mme wangu mme wangu lakini hakuitika, nlijua labda ananitania ilibidi nimfate chumbani, nlimkuta amelala chali miguu chini akiwa hajavua viatu, ilikuwa kawaida yangu kila siku kumvua viatu kwa sababu tayari nlishakubali kuwa mjinga kwake ili kulinda ndoa yangu. Nliteremka chini nkiwa katika hali ya unyonge, nkamvua viatu vyake pamoja na soks, nlisogea na kumuuliza tena machozi yakiwa yananilenga lenga.

"Mume wangu, uko serious kwa ulichonambia au unantania!?....
"Siitaji kuongea chochote niache nipumzike. alisema kwa mkato.
"Mume wangu hali yangu si nzuri nambie ukweli basi, please ongea chochote kile chengine kizuri nionee huruma mwenzio. Nilisema kwa sauti iliyokuwa imejaa upole.
"mwanamke nielewe, siitaji kuzaa kwa sasa. Alisema.

Niliumia sana kusikia hivyo kwa mara ya pili machozi yalianza kunitoka kama mtoto, aligeuka na kulalia tumbo nkasikia akisema maneno yaliyonifanya nikate kulia.

"Tena hiyo mimba nataka uitoe haraka iwezekanavyo.
"Unasemaje masoud!!? ,, nlimuuliza kwa mshangao.

"sii matangazo ya vifo umepewa masikio ili kusikia. Alijibu kwa kunikejeli.
"Masoud unanijibu hivyo mimi leo! kwa kipi kibaya hasa nlichokufanyia?....

kwanzia siku hiyo alianza kubadilika, nyumbani alikuwa akirudi muda  anaotaka, ilifika kipindi akawa analala chumba chingine nkimuuliza kwa nini anasema Toa mimba.

Toa mimba ndo ukawa wimbo ulobakia nyumbani, hakukuwa na salama tena kisa mimba, nkafika sehemu nkachoka maneno yake. nakumbuka alikuwa anajiandaa kwenda kazini nlimwambia naomba niende clinic kuandikisha.

Aligeuka na kuniangalia, akaniuliza nasemaje? nkarudia tena nlichomwambia, aliniangali bila kupwepwesa macho zaid ya sekunde nne kisha akasema.
"Nimesema!, toa, hiyo, mimba. 
"Hivi masoud kwa nini unakuwa hivi mume wangu ee, kuna familia inaitaji watoto, kuna wanawake hawajapewa kizazi wanalia kila siku mtoto, leo mimi nimejaaliwa kupata mimba unasema nitoe kwa nini lakini?, tena ni ya halali mume wangu hatujazini sisi au ulinioa kwa ajili ya starehe zako binafs?.
"Yyees nlikuoa kwa ajili ya Starehe, alisema masoud kwa hasira.. na bora ningeoa gumba hazai kwa sababu siitaji kuzaa. kwa nini ung'ang'anie wakati staki lakini. siitaji kuzaa mwanamke siitaaajiii kwani lazima!? na usipoitaji kutoa hiyo mimba mtafute baba yake mimi sio.
"Masoud naomba usinifanyie hivo, kwa nini lakini unanifanyia hivyo mimi, kwani  kitu gani hasa kikubwa kinakufanya hivyo ee!. Nlianguka chini nkamshika mguu.

Sikuamini kama masoud anaweza kunipiga siku moja, lakini siku hiyo kudhiirisha kuwa hayuko tayari kuzaa na anaichukia mimba yangu, alinigeukia akanisukuma kitandani na kuanza kunipiga ngumi za tumbo huku akilalamika kwa kunambia.

"kwa nini hunielewi wewe mwanamke, au mpaka nikuue ndo uamini, sitaki, Sitaki, Sitaki, sitaki mpumbavu wewe,sasa kwa kuwa hutaki kutoa ngoja niitoe mimi, alaaaa unanletea upuuzi hapa!.

kila aliposema Sitaki, alikuwa akinikandika ngumi za tumbo zilizopelekea kuzimia.
jasho lilikuwa likimtoka, aliniacha bila kujali akaenda kazini, nlipozinduka nlishangaa kuona tumbo linaniuma sana, nlitoka nkaenda hospitalini, docta alinipima akanipatia dawa na kunishauri nipumzike.
Nlirudi nyumbani nkiwa natokwa na machoz. kibaya zaid nlikuwa sijui kwa nini masoud alibadilika kiasi hicho, kiukweli nliumia sana, nlihisi dunia ni chungu ndani ya muda mfupi, nlitamani kufa kwa hali nliyokuwa nayo. Bado sikuacha kumjali mume wangu, niliamini ipo siku mungu atanisaidia na kama mali ndo zimemfanya awe hivyo basi atamkumbusha kuwa anakosea, atajirekebisha.

Mwanangu!. ulikuwa ni usiku wa tarehe mbili siku ambayo sitoisahau katika maisha yangu, alikuwa ameingia bafuni kuoga, cm yake iliita nikasogea karibu kuiangalia nkakutana na jina Yulai'na kwenye screen.

nilishtuka kidogo baada ya kuangalia saa nkakuta ni saa tano usiku, nikajiuliza ni nani huyu anaempigia mume wangu usiku wote huu. nlinyanyua nkapokea, nikaweka sikioni kisha nkakaa kimya kusikia ataongea nini.
Moyo wangu ulianza kuuma na kujuta kwa nini nimepokea nliposikia akisema "Hello Darlin how are you!!
sikuongea chochote nkijua uenda ataongea kitu zaid ya hicho, na kweli baada ya kuona nimekaa kimya akasema. 
"Switty! mbona kimya! , au uko na hicho kijimwanamke chako?, ila kama nlivyokuambia naomba usifanye nacho mapenzi. siitaji masoud siitaji, ikifika asubuhi kabla ya kuingia kazini njoo upate vitu vitamu huku ambavyo hakajawai kukupatia si unanijua shuguli yangu?. habari nzuri ambayo nadhani ni kiunganishi kizuri cha mapenzi yetu nimeenda kupima leo nimeambiwa nna kabeby tumboni natamani uwepo ukashike shike katumbo kangu.

sikuweza kuvumilia, miguu ilishika ganzi nkaishiwa nguvu, nlifanikiwa cm kuiweka kwenye meza nkaanguka chini.

Alipotoka bafuni aliniita huku akinimwagia maji ya baridi, nlishtuka nkalala kitandani, aliniuliza kulikoni nkamwambia hakuna ni mshtuko tu, kabla sijamaliza kuongea cm iliingia tena, aliichukua na kutoka nayo seblen, ikabidi nami nisogee nisikie atachokiongea.

"Hello Yu beib. Alisema masoud.
"mbona cm yangu ulikata?
"acha jokez bhna mi nlikuwa naoga beib nambie.
"Sina la kukuambia zaid ya kukuambia tena kesho asubuhi pita uje ukaage katoto kako tumboni nimeenda kupima nna pregnancy.

"Weeeee Sema akyamungu!.
"Akyamungu switty nna mimba yako .
"Heheheeee We mtoto mbona unataka kunifanya nimkimbie huyu mwanamke?. sii kesho nakuja sasa hivi kukaangalia kabeby kangu, Sasa hivi nakuja sawa mamaa!
"Aya njoo switty ntakuwa na amani zaid.
"Niko kwa ajili yako mmmwwaaaa!

alikata cm na kuja haraka chumbani, mimi nlimuwai nkakaa kitandani, alianza kuvaa nkamuuliza unaenda wapi sasa hivi? ,, alinijibu kwa kunambia.

"Haikuhusu.
nlishindwa kuvumilia, nlitoka hadi mlangoni na kumwambia Masoud huendi kokote, alinangalia na kunambia mara tatu naomba unipishe nipite, akaanza kunipiga makofi ya masikio, alinisukuma nkaangukia chini akapita na kuondoka zake.

Nlianza kulia kama mtoto, siku hiyo sikujua nlilala saa ngapi, aliporudi siku ya pili tayari nlishaandaa chai. nilimkaribisha vizuri kama mtu asiejua chochote, nkamuuliza kwa kujiamini nkiwa katika hali ya kawaida.
"Mke mwenzangu hajambo?
"Nini? alishangaa sana kumuuliza hivyo.
"Marudio jumaa mosi kama hujasikia limepita karibu unywe chai.
Ilibidi nimjibu vibaya siku hiyo kutokana na hasira nlizokuwa nazo kwa sababu nlishaona tayari nnakoelekea ni kubaya, nlijutia kwa nini masoud alipata mali, kwa kuwa tayari nlishajua kuwa kuna mwanamke mwenzangu ambae sikujua kama ameoa au laa, ilibidi nipunguze wivu kibaya zaid nkajua hayuko tayari kuzaa na mimi ila yupo mwanamke mwengine ambae yuko tayari kuzaa nae.
Nlipomjibu hivyo aliniuliza.
" Naona una hamu ya kupigwa sio e.
" Nshazoea kupigwa kwa sababu umenigeuza ngoma sasa hivi, kila ukijisikia unapiga tu.
Aliniangalia kwa jicho chafu, aliachia msonyo na kuingia ndani, nami nlimuangalia kwa nyuma, nkasema.
" utasonya sana mwaka huu nshaujua ukweli wala hunibabaishi, japo naumia lakini ntafanyaje.
nliongea kwa kujipa moyo lakini maumivu bado yalikuwa yakinisumbua, machozi yalianza kunitoka upya, nlimimina chai nkajaribu kunywa lakini hakikunyweka nkasukuma kikombe huko kwa hasira...

Matukio kila siku alizidi kunifanyia mapya, nlikuwa nkienda kupima hospital kila kukicha, madocta walinipa ushauri mzuri namshukuru Mungu, kwa kuwa ndo ilikuwa mimba yangu ya kwanza nlifatilia ushauri wao mwanzo mwisho, nlienda kwa wataalam wa ushauri ili kurudisha amani ndani ya ndoa yangu lakini haikuwezekana, nlipoenda kwa wazee wake kumbe tayari alishawambia wote  kuwa anataka kuoa mke mwengine ambae ndo mwema kwake na mjanja, walinishambulia kwa maneno tofauti tofauti mabaya, nkawa mtu wa kulia kila siku kila kukicha.

Mwanangu ilikuwa ni siku nyingine tena mbayo sitoisahau katika maisha yangu, nlipokuwa jikoni napika aliniita nami nkaitika, nlitoka jikoni nkaenda seblen na kukutana na sura ya mwanamke aina ya kiarabu.
nlimuangalia huku mme wangu akiwa amekaa kwenye kiti anatingisha miguu, nlimsalimia mume wangu na kumwambia huyo dada karibu. kilichonishangaza baada ya kumwambia hivyo alinisonya akanishusha na kunipandisha. mume wangu alicheka sana,  moja kwa moja nkajua uenda huyo ndo Yulaina.

"Najma, aliniita masoud nami nkaitika.
"Abee. Kwa upole.
"Huyu anaitwa Yulaina mtoto mzuri kuliko wote duniani , mtoto wa kiarabu, mtoto mwenye hadhi ya kukaa kwenye nyumba nzuri kama hii. Yani alivyoingia tu na nyumba imecheka kwa sababu ameendana nayo, kama unavyomuona akikaa kwenye sofa anajaa kama jini vile Heheheee vipi tumependeza ee!!!. Alisema.

sikuweza kuvumilia, hasira ziliniingia nkamwambia basi inatosha, nlitoka pale na kuingia ndani chumbani,  nkapakia nguo zangu kwenye begi machozi yakiwa yananitoka, hapo tayari nlikuwa na mimba ya miezi mitano na nusu. Nilitoka ndani hadi seblen mwili wangu ukiwa hauna nguvu, nlijaribu kufuta machozi yaliyokuwa yanatoka lakini ilishindikana, nkiwa na begi nlimuangalia masoud nkamwambia.

"Asante Sana, Nashkuru masoud, Mungu akuongoze, Nshallah atanilipia kwa yote nliyokufanyia kama mke, na hiki kiumbe kilichoko tumboni ipo siku moja utakifata tu hali ya kuwa hakikutambui, na hicho kiungo kilichoko mwilini mwako kitakutafuna tu.
Aliniangalia akiwa anacheka, kabla sijatoka nje aliniita na kunambia.
" Cha kukusaidia tu ngoja nikuandikie Talaka zako zote tatu na usahau kuhusu mimi kwa sababu hatuendani, lengine kama hutojali, najua pakuishi patakuwa tabu kidogo kwa sababu huyo mama yako ana kanyumba kana chumba kimoja tu, tena si kanyumba nimekueshim kijibanda,  nakuachia shamba la huko kijijini uishi humo na ni lako hilo nimekupa, nnavyokupenda na mkataba wake huu hapa, nakupatia bure si langu mimi hilo silitambui ila tu ntakuja kuvuna kila kilichomo ili upande vya kwako, wasalimie Siwezi kuwa na mwanamke wa kiswahili mimi mshamba mshamba tu, naitaji mwanamke anaejua kutumia bhana, mtoto mzuri huyu hapa kwanza kimahabba humshiki, akiwa kitandani anashugulika kweli, sii wewe dakika mbili eti mume wangu nimechoka, mashine hii hapa toto kuanzia mwili hadi ladha ni switty, sii wewe unaniita switty huku hujui kitu.

"Nashkuru Sana Masoud.

ndo jibu nlilompa baada ya kunambia aliyonambia, nlitoka nje na kukutana na kundi la ndugu zake wote, waliniangalia na kuachia kicheko nkapishana nao wakiingia ndani, nlisikia kauli tofauti tofauti wakizisema, moja ambayo nliishika mpaka kesho.
" yamekushinda ondoka usiwabane wanao weza kuyahimili.

nlitoka na maumivu makubwa sana ambayo sitoyasahau hadi kufa kwangu, na hakuna siku ntayoumia kama siku hiyo katika maisha yangu yote.
machozi yalizidi kunitiririka wakati wote, nlipofika getini nlikutana na mlinzi wa geti,  tayari nae alikuwa analia kutokana na huruma aliyokuwa ananionea, kwani nliishi nae vizuri na kumchukulia kama ndugu yangu, alinikumbatia na kuomba nimpatie namba yangu ya cm, nlimpatia akatoa kiasi cha laki moja akanipatia, nlishukuru sana kiukweli huku akinambia maneno ya mwisho.

"Sitoweza kupata bosi aliekuwa na huruma kama wewe, ntakukumbuka daima, ila konga moyo wanaume ndo tulivyo hasa tukisha pata pesa. Nilikuchukulia kama dadaangu wakati ni bossi wangu, nimeshuhudia mengi ukifanyiwa ndani lakini ulivumilia, muda wote nlikuwa nkikuonea huruma bosi unavyoteswa na mumeo, ila ya waswahili hatimae yametimia, Kiukweli nami nahisi sitoweza kuendelea na kazi hapa, bora nikose kibarua kwa ajili yako madam, naomba unisubiri hapo nje niende nimwambie nimeacha kazi ili japo tuongozane nipajue utapoishi kwa sasa, tuendeleze udugu wetu sababu umenisaidia mengi sana ambayo yalinifanya nikuone wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao bado wapo katika dunia hii ya sasa, naomba unisubiri madam niende kuaga niache kabisa hii kazi, kama kibarua nitapata kwengine tu.

KAMA UMEPITWA NA SEHEMU ZA MWANZO ZA SIMULIZI HII >BOFYA HAPA < 

TUKUTANE SEHEMU YA 06 KESHO, PITA KWENYE APP YETU KILA MUDA KWA HABARI MOTO MOTO.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.