Shilole Atoa Sharti Hili Zito Ikitokea Amekufa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Atoa Sharti Hili Zito Ikitokea Amekufa

Mwanamuziki maarufu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ametoa sharti zito kuwa, siku akifa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwembwe kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kama wanavyofanyiwa mastaa wakifariki na badala yake mambo yote yamalizike msikitini.

Siku chache baada ya video queen, Agness Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia kisha kuagwa viwanjani hapo, Shilole alisema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.

“Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa na kuuza pombe,” alisema Shilole.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.