Shilole Akanusha Kuvujisha Video Tata ya Nandy na Bilnass - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Akanusha Kuvujisha Video Tata ya Nandy na Bilnass

Mwanamuziki wa bongofleva Shilole amefunguka na kukanusha taarifa za kuwa yeye ndie aliweka picha na video ya Nandy na Bilnass katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa post aliyokuwa ameiweka katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni ya mzaha na utani tu.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo, Shilole anasema kuwa inawezekana kuna mtu anaweza kuwa ndie aliyevujisha video hiyo lakini alipoona Shilole amesema imekuwa ni kama amepata kisingizio kuwa ndie aliyefanya hivyo.

"Hamna kitu kama hiyo, mimi nilikuwa nimeweka tu ili kutania kama vile ambavyo unaweza kumwambia mtu kesho utakufa na kweli kesho anakufa kwa hio inaonekana ndio wewe kumbe watu tayari walikuwa na mambo yao. lakini ukweli sijawahi kuziona na wala sihusiki kabisa. inawezekana ni mtu ametembea na link na kutafuta sababu.

Mashabiki katika mtandao wa instagram wamekuwa wakimtuhumu Shilole baaada ya kusema kuwa alikuwa na picha nyingi za faragha za wawili hao hivyo mashabiki wamehisi hata hiyo video itakuwa iliwekwa na Shilole.


APP YETU IMEBORESHWA SASA UNAWEZA KUPAKUA UPYA KWA >>KUBOFYA HAPA<<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.