Rihama Amwaga Chozi kwa Uchungu Ataka Waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu Wamuombe Radhi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rihama Amwaga Chozi kwa Uchungu Ataka Waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu Wamuombe Radhi

Muigizaji Nguli wa filamu za Kibongo Rihama Ali amejikuta akitokwa na machozi na kulia kwa uchungu live wakati akihojiwa kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa na clouds baada ya kupata matusi na kuzarauliwa na mashabiki zake baada ya kukosa tuzo hizo.

Rihama amesema kitendo walichomfanyia waandaaji wa Tuzo za hizo akikumfurahisha na hatokisahau maishani mwake kwakua heshima inashuka wakati hakuhusishwa katika tuzo hizo toka zinaanza matokeo yake wanaamua kuandaa shindano kwa lengo la kumshusha heshima.

"Nimeumia sana sana lengo lao ni kunishushia heshima mimi sikujua lolote linaloendelea chakushangaza naambulia matusi kutoka kwa mashabiki zangu mimi Tamko langu nataka waniombe Radhi sivyo wasinihusishe kwenye tuzo zao na hata wasije kunipa tuzo ya heshima hata nitakapokufa' alisema Rihama

' Hata kama walikua na mambo yao wangefanya bila ya kunihusisha mimi' mimi ni brand ambassader wao wanataka kuniharibia kazi yangu mimi sideal na mtu kwanini wanataka kunizibia riziki yangu kazi yangu ndo inanisaidia kulea familia yangu nimeumia na hili kovu halitakuja kufutika na linaweza kunivunja moyo nikaona makubwa niliyofanya si kitu na kama hawataniomba radhi wasiniusishe milele.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.