Ray C Awatolea Povu Wote Waliomkejeli Wakati Kibonge, Awaita .... - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C Awatolea Povu Wote Waliomkejeli Wakati Kibonge, Awaita ....

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Rayc amewatolea povu zito watu wote ambao waliowahi kumsema kuhusu ubonge wake siku za nyuma.

Rayc ni moja kati ya wasanii wa kike ambao miaka kama kumi iliyopita enzi za ustaa wake alikuwa anavutia sana hadi kufikia hatua ya kuitwa kiuno bila mfupa.

Lakini alinenepa sana miaka ya hivi karibuni baada ya kuacha kutumia madawa ya kulevya kupelekea watu kumkejeli alipokuwa anashindwa kukata mauno kama zamani kutokana na mwili mkubwa.

Lakini Ray C amepunguza kilo nyingi tu na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha yake inayomuonyesha akiwa mwembamba kupita kiasi ambapo ameweka picha hiyo na kusindikiza kwa maneno haya:

"Wale wote walionikejeli nilivyonenepa mat.. yenu!"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.