Rammy Galis “Aggy Uliniambia Huwezi Kunipenda Nikikataa Kupima Ngoma” - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rammy Galis “Aggy Uliniambia Huwezi Kunipenda Nikikataa Kupima Ngoma”

Muigizaji Rammy Galis ni moja kati ya mastaa wa Bongo walionyesha kuguswa na kifo cha Agnes Masogange ambaye ni mpenzi wake wa zamani, Rammy Galis ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe ambao umemuumiza kutokana na taarifa hizi.

“Mkono umekuwa mzitoo hata kuandika maumivu niliyonayoo naona nashindwa . Dunia tambara mbovu , unadeki salama mchana usiku unakua mmbovu umenifunza mengi niliyokua siyajui , ulisema nishkuru mungu watu wakikupenda kwani adui haumjui”

“Miezi 11 tumeishi nashkuru ulinipeleka kupima ( Palestina ) , Nilitokwa na jasho ukanicheka ukaniambia huwez nipenda kama nikikataa kupima magazeti ya udaku walipotaka sababu sikuweza kuweka tofauti zetu hadharani kwani bado moyoni niliamini ipo siku Tungeweza Kumuepusha shetani . Tulikesha Usiku Na Mchana ili Ucheze Filamu Yetu Kwa hisia ” Ukasema Hii Iwe Kumbukumbu Yako Kama Niliwahii Hata Kwenye Kazi Zako Kukusaidia”
“Sasa kwanini filamu yetu tulitunga jina liitwe #HUKUMU ? Ilikuwaje Story ya filamu mwisho unafariki ? kwani tulikua tunatungia iwe kweli Hukumu yako ???? Mungu ndio hakimu wa viumbe vyote katika dunia , umeondoka ghafla sanaa , Na hii pia ni funzo umeniachia #PumzikaSalama #MileleNakuombea#RIPLOVE😢”

Marehemu Agness Masogange enzi za uhai wake aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Rammy Galis kwa kipindi kifupi kinachotajwa kufikia miezi 11 lakini baadae waliachana na kutotaja sababu ya kuachana kwao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.