Pesa Yamtoa Mwigizaji Salman Khan Katika Kifungo cha Miaka 5, Akaa Jela Siku 2 Apewa Dhamana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Pesa Yamtoa Mwigizaji Salman Khan Katika Kifungo cha Miaka 5, Akaa Jela Siku 2 Apewa Dhamana

Siku mbili baada ya Mahakama nchini India kutoa hukumu ya miaka mitano kwa Staa wa filamu nchini India Salman Khan kwa kosa la ujangili mwaka 1998, staa huyo ameachiwa huru kwa dhamana.

Khan ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kukata rufaa, ikiwa ni siku mbili baada ya kulala jela na mahakama kumwamuru alipe faini ya Dola za Marekani 154 sawa na takriban Shilingi za Kitanzania 369, 600.

Khan anadaiwa kuua swala wawili wa aina ya ‘blackbucks‘ ambayo hulindwa sana nchini humo. Alifanya kosa hilo katika mji wa Rajasthan wakati wakitengeneza filamu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.