Nedy Music Azungumzia Suala la Kufanya Kazi na Alikiba Pia Kusaini WCB Wasafi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nedy Music Azungumzia Suala la Kufanya Kazi na Alikiba Pia Kusaini WCB Wasafi

Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amefunguka kuhusu mipango yake ya kufanya kazi na Alikiba pamoja na kusaini katika label ya WCB.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘One and Only’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mipango ya kufanya ngoma na Alikiba ipo ila anahitahitaji watu wamjue kwanza na sio wafanye kwa sababu wanajuana.

“Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea,” amesema.

Kuhusu kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.

PKP ni label ambayo inamilikiwa na msanii Ommy Dimpoz ambaye July 06, 2017 alisaini kufanya kazi na label ya RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.