Ndoa ya Alikiba Ratiba Yaanikwa, Mambo Yatakuwa Hivi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ndoa ya Alikiba Ratiba Yaanikwa, Mambo Yatakuwa Hivi

Muimbaji nguli wa nchini Tanzania, Alikiba amesafiri pamoja na familia yake Jumanne hii (April 17, 2018) kuelekea mjini Mombasa nchini Kenya kwaajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh itayofanyika April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa nchini humo.

Taarifa za ndoa yake ziligubikwa na usiri mkubwa hali ambayo ilivifanya vyombo vingi vya habari nchini Tanzania na Uganda kuandika tetesi za ndoa hiyo huku vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai ndoa hiyo ilishafungwa.

Bongo5 iliamua kulivalia njuga suala hili ili kutafuta ukweli wa ndoa hiyo ndipo ukweli ulipobainika kwamba muimbaji huyo anafunga ndoa April 26, 2018 na siku ya jana amesafiri pamoja na familia yake kwenda Mombasa Kenya.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, ndoa hiyo itarushwa live na kituo cha runinga cha Azam TV baada ya kununua haki ya kurusha ndoa hiyo kwa kiasi kinachodaiwa ni zaidii ya milioni 100 za Tanzania.

Baada ya kumaliza kwa ndoa hiyo nchini Kenya, Muimbaji huyo atafanya sherehe nyingine nchini Tanzania wiki moja baada ya ndoa ya awali.

Chanzo hicho kimedai ndoa hiyo itagharimu mamilioni ya hela kutokana na maandalizi pamoja na deal hilo la Azam. 


>BOFYA HAPA< KUPAKUA APP YETU MPYA ILIYOBORESHWA ZAIDI

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.