Mtoto wa Ronaldo Aanza Kuweka Rekodi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mtoto wa Ronaldo Aanza Kuweka Rekodi

Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Club ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo sasa ni wazi kuwa amepata mrithi sahihi katika kazi yake ya soka Cristiano Ronaldo Junior, Ronaldo JR ameanza kuchukua headlines akiwa bado ana umri wa miaka 7.

Kama hufahamu Cristiano Ronaldo Junior ni mtoto wa kwanza wa Cristiano Ronaldo ana umri wa miaka 7 na sasa ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kushinda tuzo mbalimbali akiwa bado ana umri wa miaka saba.

Ronaldo Junior April 14 2018 akiwa na bibi yake mzaa baba Dolores Aveiro ameshinda tuzo ya kuwa mfungaji bora wa shule baada ya msimu kumalizika, hiyo ni tuzo ya kwanza ya Ronaldo Junior kupata katika soka na Ronaldo na mama yake wote wamepost katika account zao za instagram kumpongeza Ronaldo Junior.

Kwa upande wa baba mtu mwenyewe Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi 5 kubwa Ulaya (391), UEFA Champions League (120), UEFA European Championship (29) na FIFA Club World Cup (7) na ndio mchezaji aliyefunga magoli mengi UEFA Champions League katika msimu mmoja (17).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.