Mrembo Tunda Akana Skendo Za Kubeba Mimba Ya Diamond na Mastaa Wengine - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mrembo Tunda Akana Skendo Za Kubeba Mimba Ya Diamond na Mastaa Wengine

Video vixen maarufu Tunda Sebastian ambaye amewajia kuonekana kwenye videosa wasanii kama Young Dee, Country Boy na wengineo amekataa tetesi za kutoa mimba za mastaa wengi Bongo.

Tunda ameshawahi kuandamwa sana na skendo za kuchoropoa mimba kadhaa huku mimba nyingine zikidaiwa zilikuwa za staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Lakini tetesi hizo zilizpamba moto Miezi michache iiyopita baada ya Tunda kuonekana akiwa amenenepa na kuwa na tumbo kubwa taarifa alizodai kuwa alinenepa kwa sababu anapenda kula sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews ya East Africa Tv, Tunda amekataa na kudai sio mjamzito na wala hajawahi kushika ujauzito na wala kutoa ujauzito wowote:

"Nani mjamzito? Mimi sio mjamzito kwa sababu muda haujafika wa mimi kuitwa mama lakini siku ikifika nitafurahi kuitwa mama lakini mambo hayo ya mimi kutoa mimba ni stori za mitandaoni lakini sio kweli mambo mengi yanaongelewa lakini hayana ukweli”.

Tunda hivi sasa yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa Kituo cha Clouds Tv Casto Dickson ambaye ameweka wazi nia yake ya kumuoa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.