Mourinho Kakubali Yaishe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mourinho Kakubali Yaishe

Jose Mourinho amesema kwa sasa anachoweza kuwahakikishia mashabiki wa Manchester United ni timu yao kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England maana kuikamata Manchester City kimekuwa kitu kigumu kwelikweli.

Mourinho alisema Man City imeonyesha utawala kwenye Ligi Kuu England msimu huu na hata kama timu yake itashinda haiwezi kusaidia kitu kwa sababu vijana hao wa Pep Guardiola, nao wanashinda tu.

Man United ilifanikiwa kuiondoa Liverpool kwenye nafasi ya pili baada ya juzi Jumamosi kuichapa Swansea City 2-0 huko Old Trafford, wakati mapema tu kikosi cha Jurgen Klopp, kiliichapa Crystal Palace 2-1, shukrani kwa mabao ya Sadio Mane na Mohamed Salah, yaliyowafanya kuketi nafasi ya pili kwa muda.

Mourinho anaamini kikosi chake cha Man United kipo vizuri kuliko timu nyingine zote ukiwaondoa Man City na mwenyewe amekiri si watu wepesi kuwafukuzia.

“Msimu uliopita, tulishinda taji lakini tulimaliza namba sita kwenye ligi,” alisema Mourinho.

“Tunataka kumaliza wa pili msimu huu na tumevuna pointi 10 zaidi ya msimu uliopita, tumefunga mabao mengi na tumeruhusu machache, lakini kuna klabu imeonekana kuwa vigumu kuikimbiza. Kwa ligi nyingine, tungekuwa tunafukuzia ubingwa.

“Tumekuwa na msimu mzuri na bado tunaweza kushinda Kombe la FA. Tutaendelea kupigania kwenye hilo.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.