Mohamed Salah Ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwaka Huu PFA 2017-18 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mohamed Salah Ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwaka Huu PFA 2017-18

Mohamed Salah ndiye mchezaji anayeongoza kwa magoli katika Premier League msimu huu

Mohamed Salah ameshinda tuzo la mchezaji bora la Shirikisho la wacheza soka ya kulipwa mwaka 2017-18.

Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25, amemshinda Kevin de Bruyne, Harry Kane, Leroy Sane, David Silva na David de Gea katika kura iliyopigwa nwa wachezaji wenzake.

Mchezaji wa Manchester City Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana , huku naye mchezaji wa Chelsea Fran Kirby ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwanamke wa mwaka huu.

Lauren Hemp wa Bristol City ametajwa kama mchezaji bora kijana mwanamke wa mwaka huu.
Sane played alikuwa na jukumu kuu katika kushinda kwa Manchester City taji la msimu huu

"Ni heshima kubwa na hususan kwamba ni kura iliyopigwa na wachezaji. Naskia raha na sifa kubwa," Salah amesema.

"Sikuapta nafasi nilipokuwa Chelsea. Ni wazi kwamba ningerudi na nionyeshe kila mtu soka yangu. Nadhani niliondoka na nimerudi nikiwa mtu tofuati, na mchezaji tofuati. Naskia raha sana na sifa pia."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana "furaha ya kuwa na nafasi hiyo " yakuwa meneja wa Salah na kuongeza kwamba ni 'haamini amepata heshima hiyo' ya kushinda tuzo hilo.
'Kila anachogusa kinaishia wavuni'

Salah amefunga magoli 31 katika mechi 33 kwa timu ya Liverpool iliyo chini ya ukufunzi wa Jurgen Klopp' na anogoza kushinda tuzo la the Golden Boot.

Goli la 31 la raia huyo wa Misri dhidi ya West Brom siku ya Jumamosi lilimueka sawa na Alan Shearer, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez, wanaoshikilia rekodi hiyo kwa mechi ya 38 ya msimu.

Alifunga katika mikondo yote ya mechi ya ilioipa Liverpool ushindi wa 5-1 dhidi ya Manchester City katika robo fainali ya ligi ya mabingwa, pamoja na magoli manne katika ushindi wao wa ligi dhidi ya Watford mnamo Machi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.