Mama Mobeto Ataka Mtoto Wake Aolewe na Mzungu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mama Mobeto Ataka Mtoto Wake Aolewe na Mzungu

Mama mzazi wa mwanamitindo na video vixen Hamisa Mobetto alifunguka hivi karibuni na kusema kuwa alitamani sana mtoto wake kuolewa na mzungu. Mama huyo anasema kuwa lengo kubwa la yeye kuolewa na mwanaume wa kizungu ni kutokana na kuamini kuwa wanaume wengi wa kiafrika hawana mapenzi ya kweli.

Akiongea na MCL Digital, mama mobeto anasema kuwa anaamini kuwa mtoto wake ni mrembo na ana sifa za kuolewa na mwanaume mwenye kumjali na kumpenda.

"unajua mtoto wangu mzuri, mrembo na anashingo ndefu nataka mwanaume atakae muoa amwangalie kama malaika, amwangalie kama malaika kwa sababu ni mwanamke mwenye msimamoyake na ametulia sio kama watu wanavomfikiria"
wazungu hawana stress, wanajua kujali na kumpenda mwanamke , hawanaga longolongo hasa linapokuja swala la mapezni tofauti sana na wanaume wa kiafrika."

Akiongelea swala la mtoto wake kuzaa na wanaume tofauti tofauti, mama mobeto anasema kuwa kwake haina shida kwa sababu yeye alibahatika kumzaa mtoto mmoja tu na hivyo anaona kabisa kuwa bora amleteee watoto wengi maana hao ndio ndugu zake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.