Madonna Ashindwa Kesi ya Barua ya Kutemwa na Tupac Shakur Kuuzwa Mnadani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Madonna Ashindwa Kesi ya Barua ya Kutemwa na Tupac Shakur Kuuzwa Mnadani

Malkia wa muziki wa Pop kutoka nchini Marekani na mshindi wa tuzo za Grammy, Madonna ameshindwa kesi ya haki ya kulinda kutotolewa kwenye jamii kwa mambo yake binafsi na marehemu Tupac Shakur.

Mwaka jana, mwana mama huyo alikwenda mahakamani kuzuia mnada uuzwaji wa barua ya kutemwa na Tupac. Hata hivyo, jitihada zake hizo zimegonga mwamba.

Barua hiyo ambayo iliandikwa na hayati Tupac ambaye alikuwa mpenzi wa Madonna katika kipindi ambacho hakikufahamika, inatarajiwa kuuzwa kwa mnada mwezi Julai mwaka huu.

Tupac aliandika barua hiyo kwenda kwa ex wake huyo Januari 15, 1995 ikiwa ni miezi 18 kabla ya kifo chake. Sasa barua hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa kianzio cha dola 100,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 228 za Kitanzania.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.