Lulu Diva Adondosha Chozi Hadharani, Kisa... - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Diva Adondosha Chozi Hadharani, Kisa...


MWANA-MUZIKI Lulu Abass ‘Lulu Diva’ hivi karibuni alidondosha chozi mbele ya wanafunzi wa Shule ya Lord Baden iliyopo Bunju jijini Dar alipokuwa amewatembelea na kilichomtoa machozi ni kumbukumbu za yeye kushindwa kusoma.

Lulu alimwaga machozi alipokuwa akitoa wosia kwa wanafunzi hao kuhusiana na masomo kwani yeye hakupata nafasi ya kusoma kama wao licha ya kwamba alitamani kusoma ili aufanye muziki vizuri zaidi.

“Nikiwaona hivi mpo shule na mimi natamani sana nirudi shule kwa sababu muziki bila elimu ni shida, nyie mliopata nafasi hiyo mjitahidi sana kuzingatia masomo maana hakuna chochote kinafanyika bila elimu,”
alisema Lulu Diva huku machozi yakimbubujika

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.