JB: Tasnia ya Filamu Haijafa, Hayo ni Maneno Ya Wavivu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

JB: Tasnia ya Filamu Haijafa, Hayo ni Maneno Ya Wavivu

Mkongwe wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amesema kimsingi tasnia ya filamu Bongo haijafa kama wengi wanavyodhani.

JB alisema wavivu ndiyo wanaolalamika kwamba tasnia imekufa na hailipi jambo ambalo halina ukweli wowote.

“Mimi nasikia tu kwamba watu wanasema kuwa tasnia hailipi lakini mimi inanilipa vizuri ndiyo maana tunahitaji wasanii ambao wapo vizuri kwa mfano Gabo nilicheza naye kwenye filamu ya Danija na ikafanya vizuri, Shamsa Ford nilicheza naye kwenye Zawadi Yangu na ikafanya vizuri, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kama tukizidi kuongeza juhudi,” alisema JB.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.