Hizo Ndio Dalili Zitakazo Kuonyesha Kuwa Mwanaume Amekuchoka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizo Ndio Dalili Zitakazo Kuonyesha Kuwa Mwanaume Amekuchoka

Uhusiano sio kitu kirahisi kinahitaji kazi kwani pale mnapokutana watu wawili wenye tabia tofauti, mitazamo tofauti kukinzana lazima lakini nini hutokea pale mwanamke unapokuwa unampenda sana mwanaume wako halafu ghafla unakuwa humuelewi?
Leo naomba niwaambie wanawake kwamba mwanaume akikuchoka ujue basi tena ujue uhusiano umekufa na kujaribu kuurudisha unakuwa mgumu sana, kwaiyo ufanyeje? Cha muhimu ni kutambua mapema kabla hajafika huko ili ujaribu kumuweka katika mstari ulionyooka kwa sababu usije mkosa moja kwa moja. Kwa hiyo ni muhimu kama mwanamke kujua kuwa mwanaume wako unamridhisha na anafuraha kila siku ila kuna baadhi ya dalili ukiziona ujue Hana furaha na ameshakuchoka.
Dalili zitakazokuonyesha Mwanaume ameyachoka mapenzi yenu:
1. Atafanya jambo lolote atakalojisikia.
Mwanaume akikuchoka hatajali hisia zako, hatakushirikisha kwenye maamuzi yake kwani kwani hataki uwepo kwenye mipango yake hivyo hatojali mchango wako kwenye maamuzi yake.
2. Ataanza kukasirika bila sababu
Mwanaume akikuchoka kwenye uhusiano ataanza kuwa na kisirani kisicho na sababu yaani ukifanya kitu kidogo utanuniwa, utagombezwa bila hats sababu ya msingi ujue hapo anatafuta sababu za kukuacha maana anaona kama unamkera kila wakati.
3. Atapunguza Ukaribu
Mwanaume akikuchoka yaani utajua tu kuna vitu vidogo vidogo ataacha kufanya kama vile kama alikuwa anakupigia simu mara tano basi atakupigia mara moja kwa siku. Yaani ni vile vitu alikuwa anafanya kukuonyesha anakujali vinaisha.
4. Mawasiliano Yatapungua
Mwanaume akikuchoka lazima atakata mawasiliano ataacha kukwambia yaliyo moyoni mwake kama mlikuwa mna kawaida ya kuonana ghafla ataanza kutafuta vusingizio ilimradi tu akukimbie msije mkaonana na hata mkionana anakosa kitu cha kukwambia pia ataacha kukusikiliza.
5. Mapenzi Yanapungua
Mwanaume akikuchoka maana yake mapenzi yake kwako yamepungua au yameisha kabisa hapa lazima ataacha kukwambia anakupenda na kukujali na Kama kuna ishara alikuwa anakuonyesha basi zitaisha.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.