Hii Ndio Sababu Ya Wema Kutohudhuria Mazishi Ya Agnes Masogange - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hii Ndio Sababu Ya Wema Kutohudhuria Mazishi Ya Agnes Masogange

Wikiendi iliyopita marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ aliagwa na wasanii wenzake wa Bongo movie pamoja na Bongo fleva kwenye viwanja vya Leaders Club.

Lakini Wema Sepetu alizua gumzo baada ya kitohudhuria siku hiyo wasanii wote walipoenda kisha mwili na hata wasanii waliposafiri kwenda Mbeya kwenda kumzika.

Hapo mwanzoni kuna taarifa zilikuwa zinaenea na kudai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka Wema asihudhurie mazishi ya Masogange ni kwa sababu ya bifu lili kuwepo kati yake na marehemu.

Baada ya Tetesi hizo kuenea gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Neema Ndepanya ambaye ni meneja na mtu wa karibu wa Wema ambaye alifunguka haya:

"Wema alikuwa na nia ya kufika msibani kabisa na alikuwa ameshajiandaa lakini ilishindikana baada ya kuugua tumbo la ghafla ikabidi aahirishe tu, pia Mbeya alishindwa kusafiri maana Jumatatu ambayo ndiyo mazishi ya Masogange alikuwa anatakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi yake inayoendelea".


Agnes Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.