Harmonize na Diamond na Mpango wa Kuondoa Ngoma za Nigeria Bongo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize na Diamond na Mpango wa Kuondoa Ngoma za Nigeria Bongo

Msanii wa muziki Bongo kutoka label ya WCB, Harmonize amesema ngoma yake mpya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru ni mwanzo wa kurudisha ngoma za kuchezeka.

Muimbaji ameiambia Funiko Base, Radio Five kuwa nyimbo za kuchezeka Bongo zimepungua kwani ambazo zinazotoka sasa hivi zimepoa kitu ambacho kinafanya nyimbo za wasanii wa Nigeria kupewa nafasi hasa club.

“Inafikia wakati tunaona ni lazima tucheze, so tukaona this time around tukija na Kwa Ngwaru kama ngoma nyingi zilitoka kama zimelala ndio maana ukienda club unasikia Wanigeria wakati sisi tunaweza tukafanya muziki mzuri watu wakapenda na wakacheza,” amesema.

“Mwisho wa siku tunapenda tu ngoma zao kwa sababu ya beat lakini lugha hatuijui,” ameongeza.

Kwa Ngwaru ni ngoma ya pili kwa Harmonize kumshirikisha Diamond baada ya hapo awali kumshirikisha katika wimbo iitwayo Bado iliyotoka mwaka 2016.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.