Harmonize Afunguka 'Sijawahi Kutamani Kufanya Kolabo na Alikiba' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize Afunguka 'Sijawahi Kutamani Kufanya Kolabo na Alikiba'

Harmonize Afunguka 'Sijawahi Kutamani Kufanya Kolabo na Alikiba'
Msanii Harmonize kutoka kundi la Wasafi amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hajawahi kutamani kufanya kazi na Alikiba wala msanii mwingine yoyote lakini kama itatokea huko mbeleni ataweza kufanya.

"lengo la watanzania wote ni kuona jinsi gani tunaweza ku-push muziki wetu na kuupeleka mbali, sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba au msanii mwingine yoyote yule, lakini itatokea kipindi tutafanya tu.

vitu vingine ni lazima viwepo ili mambo mengine nayo yaendelee, kwaio mimi sioni kama kuna kitu cha ajabu sana"

Hivi karibuni Harmonize aliingia katika headline baada ya kumjibu shabiki kuwa alionekana ku-mind sana Alikiba alivyompa mkono Diamond huku kwake ikionekana kama haikuwa njia sahihi ya kumpa mkono kwa sababu Alikiba aliugeuza mkono na hakutaka kumpa kupitia kiganjani.

Hata hivyo wasanii hao (DIAMOND AMBAE NI BOSI WA HARMONIZE NA ALIKIBA) kwa sasa wanaonekana kuanza kumaliza tofauti zao kutokana na kupungua kwa speed ya matusi katika mitandao lakini pia Diamond kumpa hongera Alikiba ya kuoa na pia kusalimiana katika msiba na kukaa meza moja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.