Harmonize Awasihi Mashabiki Wasimchonganishe na Alikiba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize Awasihi Mashabiki Wasimchonganishe na Alikiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘ Kwa ngwaru’ Harmonize ameibuka na kuwasihi mashabiki zake wasimchonganishe na msanii mwenzake Ali Kiba.

Kwa muda mrefu kumekuwa na sintofahamu kati ya Diamond na Ali Kiba hali iliyosababisha kuwepo hata kwa uadui kati ya wasanii wa WCB au watu wake wa karibu na watu wa karibu wa Ali Kiba.

Siku ya Jumapili kwenye viwanja vy Leaders Club Ali Kiba na Diamond walizua gumzo baada ya kusalimiana msibani kuonyesha kama hakuna tofauti baina yao.

Lakini Harmonize alikaaa pembeni ya Ali Kiba lakini kilichowashangaza watu wengi ni baada ya kuonekana hawajaongea neno hata moja yaani kiufupi walichuniana.

Baadae mashabiki walimjia juu Harmonize na kudai alimchunia Ali Kiba hakumpa hata salamu wakati bosi wake Diamond alijishusha na akamsalimia Ali Kiba.

Harmonize amemtolea povu shabiki kupitia mtandao wa Instagram na kumtaka asimgombanishe na Ali Kiba:

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.