Dogo Janja: Wanaume ni Waongo Sana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja: Wanaume ni Waongo Sana

Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chande maarufu kama Dogo Janja, amefunguka na kuwapa ushauri wanawake kuwa wawe makini na maisha na si kuwategemea wapenzi wao kwa kuwa wanaume ni waongo sana.

Dogo Janja ambaye ni mume wa msanii wa filamu, Irene Uwoya, amesema ni vyema wanawake wengi wakajiongeza na kujitegemea kwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato au kuhakikisha anajituma ili aweze kuyamudu maisha kwa ujumla.

“Wanawake watambue kuwa anayekupa hela ya kula na anayekupa kazi upate hela ya kula ni bora anayekupa kazi, huyo mwingine hakutakii mema zaidi ya kukuharibia maisha yako ya baadaye,” alisema Dogo Janja.

Alisema anafurahi kuona wanawake wengi wakijipatia fursa za kuendeleza maisha yao hali inayowafanya kujitofautisha na maisha ya zamani ambayo wengi walikua wanashindwa kutumia fursa wanazokutana nazo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.