Diamond Platnumz Kung’ara Kwenye Kombe la Dunia na ‘Colours’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz Kung’ara Kwenye Kombe la Dunia na ‘Colours’

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezidi kupaaa kwa mafanikio na kuupeleka muziki wa Bongo fleva mbele baada ya kufanikiwa kushirikishwa na Jason Derulo kwenye wimbo wa Kombe la Dunia.

Diamond na Jason Derulo msanii kutoka Marekani wamefanya kwa pamoja wimbo unaoenda kwa jina la Colours ambao umeandaliwa na kampuni ya Coca Cola maalumu kabisa kwa ajili ya kusheherekea Michezo ya Kombe la Dunia inayotegemea kufanyika hapo baadae mwaka huu.

Wimbo huo ambao umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na Ma prodyuza kutoka nchi nyingine, umedhaminiwa na kampuni ya ya coca cola Tanzania.

Wimbo huo maalum wa kombe la dunia 2018 umezinduliwa leo Katika Hotel ya Hyatt, jijini Dar es Salaam, ambapo Diamond, Nahreel na msemaji wa Coca Cola wamesema wamesha uachia hewani wimbo huo hivyo unapatikana kwenye mitandao mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliweka Ujumbe kuhusu Wimbo huo:

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.