Daimond, Nandy Baada ya Kuhojiwa na TCRA Warudi Mikono Nyuma " Ujana Maji ya Moto Haturudii Tena" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Daimond, Nandy Baada ya Kuhojiwa na TCRA Warudi Mikono Nyuma " Ujana Maji ya Moto Haturudii Tena"


Wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wamehojiwa kwa saa mbili na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Wakizungumza mara baada ya kumaliza mahojiano hayo yaliyofanyika leo Aprili 19, wasanii hao wamesema wamejifunza mengi kuhusiana na masuala ya mitandao.

Diamond amesema: “Ujana ni maji ya moto tumeelimishwa, hatutarudia tena, nitakuwa balozi kwa vijana wenzangu kuhusu masuala ya mitandao.”

Nandy amesema: “Nisameheni kwa yaliyotokea. Hapa TCRA nimepata somo kuhusu mitandao, tukio lile halitajirudia tena.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.