BREAKING NEWS: Agnes Masogange Afariki Dunia - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

BREAKING NEWS: Agnes Masogange Afariki Dunia

Video vixen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.


Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili.
Mwili wa Video Queen Agness Masogange ukichukuliwa Hospitali ya Mama Ngoma Mwenge Dar es salaam kupelekwa kuhifadhiwa Muhimbili Hospital. 
Wiki tatu zilizopita marehemu alishindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini, hii ni kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.

Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho. BongoSwaggz inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.