Baada ya Video ya Utupu Kuvuja Nadny Amtupia Lawama Bill Nass - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Video ya Utupu Kuvuja Nadny Amtupia Lawama Bill Nass

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nandy amemtupia lawama Bill Nass na kuwaomba radhi Watanzania wote waliopatwa na mfadhaiko baada ya video hiyo kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Nandy amesema kuwa video hiyo ni kweli ya kwake na Bill Nass na walipiga kipindi hicho mwaka 2016 walipokuwa kwenye mahusiano ila ameshangazwa kuona video hiyo waliyopiga wakiwa faragha kuvuja mtandaoni.

“Nilikuwa na mahusiano na Bill Nass mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi aliipataje hiyo video kwani ni lazima nimrushie ndio aipate, sijui niseme nini, Naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, mashabiki serikali yangu kwa kweli video imenichefua sana mpaka hapa ninapoongea nimechefuka, ila adhabu ya maumivu ninayoipata sasa hivi ni kutokana na kumuamini mwenzangu,“ amesema Nandy kwenye mahojiano yake na MCL Digital.

Mapema leo Aprili 12, 2018 video ya Nandy na Bill Nass wakiwa utupu imevuja kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha wawili hao wakiwa katika hali ya mahaba kitandani, hata hivyo mpaka sasa Bill Nass bado hajatoa kauli yoyote kuhusu tukio hilo na Bongo5 inafanya jitihada za kumtafuta.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.