Aunty Ezekiel Awataka Wasanii Wenzake Waache Kumlilia Kanumba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Aunty Ezekiel Awataka Wasanii Wenzake Waache Kumlilia Kanumba

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake wa Bongo movie waache kumlilia msanii mwenzao Steven Kanumba na badala yake waenzi kazi zake.

Steven Kanumba alikuwa msanii wa Bongo movie ambaye alikuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii kwani uwezo wake wa kuigiza na ubunifu uliweza kwa kiasi kikubwa kuifikisha tasnia hiyo mbali.

Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu tasnia hii ikumbuke siku ya kifo chake ambayo inaitwa Kanumba Day, Aunty Ezekiel amefunguka na kusema sasa kuomboleza kifo chake tu kumetosha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Aunty Ezekiel amesema kuwa  mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika alipokuwa amefika yeye.

"Najua wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja”.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.