Audio: Rick Ross Kufanya Kolabo na Sauti Sol, Msikie Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Audio: Rick Ross Kufanya Kolabo na Sauti Sol, Msikie Hapa

Rapa mkali kutoka wa Marekani, Rick Ross amevutiwa na kundi la Sauti Sol baada ya kuwasikiliza kwenye gari akiwa mjini Nairobi kwenye show yake ya #NRGWave anayofanyika Carnival, April 28.

Rozay ametangaza rasmi kufanya remix ya ngoma yao, to live and die in Africa baada ya kuisikia alipofika Kenya, alitangaza kwenye kituo cha radio cha NRG ambao ndio waandaaji wa Tamasha hilo.

kwenye interview hiyo ya April 27, 2018 na kituo hicho, Rick Ross alisema kuwa 'Nimevutiwa sana na wimbo wa live and die in Africa, nimeusikia wakati nilipofika hapa, na natangaza rasmi beat ya wimbo huo apewe Dj wangu ili nitie verse kwenye ngoma hiyo' wimbo huo umenigusa, nimeupenda na ni mkali.

Kupitia account yao instagram, kundi la Sauti Sol nao wameposti kipande hicho cha interview na kusema kuwa wanashukuru kwa alichofanya Rick Ross kuikubali ngoma yao na kutaka kufanya remix, na kusema kuwa wanaituma fast mchongo umalizike, Sikiliza hapo chini

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.