Alikiba Agoma Kumualika Diamond Kwenye Sherehe ya Harusi Yake Inayofanyika Dar Leo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Agoma Kumualika Diamond Kwenye Sherehe ya Harusi Yake Inayofanyika Dar Leo


Licha ya habari kusema kuwa Diamond yupo tayari kuhudhuria sherehe ya harusi ya Alikiba Jioni Ya leo hii, lakini upande wa Diamond umesema hajaalikwa. Chanzo kilicho karibu na Alikiba kimeiambia AVMEDIA.

“Kiba anaonekana bado hayuko poa na Diamond, kamfanyia mwenzake jambo la kushangaza sana maana huwezi amini hadi dakika hii hajamualika kwenye sherehe yake ya harusi, yaani inaonekana Kiba hayuko tayari kushirikiana na mwenzake maana mara nyingi amekuwa akijishusha lakini hampi ushirikiano,”

Nae Aidan Seif ambaye ni meneja wa Alikiba alipoulizwa na AVMEDIA kuhusu issue hiyo amesema.
.
“Hadi sasa hatujamualika na kwa kweli sijajua kama tutamualika,” .

Hata hivyo mastaa tofauti nchini wamealikwa. Tusubiri na tuone.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.