Agnes Masogange: Sitaki Mazoea na Mtu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Agnes Masogange: Sitaki Mazoea na Mtu

Video vixen maarufu Agnes Gerald maarufu kama Masogange amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hataki kabisa masuala ya shobo na watu baada ya kesi yake badala yake anataka kuwa kivyake.

Wiki iliyopita Masogange aliponea chupu chupu kwenda jela baada ya kuhukumiwa miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 ambayo alifanikiwa kuilipa na kuepuka jela.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Masogange alisema kuwa, kwa sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.

"Sasa hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida kabisa“.


Agnes alikamatwa mwaka jana Kwa Tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali alithibitisha hayo baada ya kumpima.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.