Wolper "Sijawahi Kuachwa na Mwanaume Kwenye Mahusiano ya Mapenzi" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wolper "Sijawahi Kuachwa na Mwanaume Kwenye Mahusiano ya Mapenzi"

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kuachwa na wanaume.

Kumekuwa na stori nyingi za kimbea mtandaoni ambazo zinaongelea kufeli kwa mahusiano ya Wolper na wanaume mbali mbali anaokuwa nao kwenye mahusiano.

Kiukweli kabisa Wolper ni moja kati ya watu waliokuwa na bahati mbaya kwenye mahusiano inawezekana ikawa pia ni wanaume ambao anachagua kuwa nao.

Kwa mwaka Jana pekee Wolper alikuwa kwenye mahusiano na wanaume watatu tofauti ambao ni Harmonize, Brown na Engine.

Lakini hivi sasa Wolper anaweka wazi kuwa mahusiano yake kuvunjika sio yeye mwenye makosa na wala hajawahi kuachwa yeye ndio anaacha kwenye mahusiano.

Wolper amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na The playlist ya Times FM ambapo ameongea Mengi zaidi:

"Kiukweli kabisa naamini kuwa hakuna siku ambayo Ex wangu hata mmoja ambaye ameshawahi kuja kuniongelea vibaya kwenye interview yoyote kwaiyo kama ningekuwa na matatizo wangekuwa wanakuja kuniongelea vibaya kwaiyo mimi na wao ndio tunajua ukweli kuwa nani ana matatizo lakini pia sipendi sana kuongelea maex ila kikubwa ambacho kipo kwangu sipendi ujinga na sipendi kuonekana mpumbavu kwa sababu mimi ni mzuri najiamini natafuta hela yangu napenda kazi yangu na napenda kuheshimiwa kwaiyo kama ukinizingua nakufuta na by the way sijawahi kuachwa"

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.