Wastara: Nipo Tayari Kuolewa Tena, Napenda Sana Mwanaume Mweusi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wastara: Nipo Tayari Kuolewa Tena, Napenda Sana Mwanaume Mweusi

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ‘Wastara Sajuki’ amefunguka na kusema yupo tayari kuolewa na kuweka wazi sifa za mwanaume ambaye anaweza kumuoa yeye na kusema anapenda mwanaume mwenye rangi nyeusi.

Wastara amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka East Africa Tv, ambapo Wastara aliulizwa ni sifa gani anazoangalia kwa mwanaume na moja kwa moja alizitiririsha.

Wastara aifunguka hayo kwenye moja ya maswali aliyokuwa anajibu aliyopewa na mashabiki zake kutokea mtandaoni.

Wastara amefunguka na kusema hivi sasa haitaji kuwa na mwanaume mweupe tena kwani ametokea kutopenda wanaume wa aina hiyo bali hivi sasa anatamani ajiopolee mwanaume mweusi ili awe naye kwenye mahusiano.

"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambaye anajiamini ambaye hata tukitembea mbele za watu hawezi kuona aibu, anayejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe mwanaume wa kweli yaani asiwe punga ila asiwe mweupe maana nawachukia sana wanaume wenye rangi nyeupe Napenda mwenye rangi nyeusi"


Wastara amesisitiza anataka mwanaume mwenye rangi nyeusi kama alivyokuwa marehemu mumewe Sajuki ambapo amekuwa na bahati mbaya na mapenzi tangu SAjuki afariki kwani ameshaolewa na kuachika mara kadhaa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.