Trump Akubali Mualiko wa Kukutana na Kim Jong Un - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Trump Akubali Mualiko wa Kukutana na Kim Jong Un

RAIS wa Marekani, Donald Trump amekubali kukutana na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un baada ya kuahidi kusitisha mpango wake wa majaribio ya nyuklia na makombora.

Kim alitoa ahadi hiyo alipokuta na Wawakilishi wa Serikali ya Korea Kusini. Hata hivyo Trump amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea hadi yatakapofanyika makubaliano

Trump na Kim wanafikia hatua ikiwa ni baada ya miezi mingi ya vitisho na vijembe walivyokuwa wakirushiana. Hii ni hatua kubwa baina ya mataifa hayo hasimu pamoja na usalama wa dunia kwa ujumla.

Marekani na Korea Kaskazini zimekua nchi hasimu kwa miaka mingi ingawa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Jimmy Carter aliitembelea Korea Kaskazini mwaka 1994.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.